Skip to main content

Open Access Africa-Swahili Version: Mwongozo wa Kunukuu Vyanzo

Miongozo Ya Kunukuu

Citation Aides

Kunukuu Vyanzo

Sehemu hii inatoa mwongozo wa kutumia mitindo tofauti kama APA na AMA katika uaandishi wa kitaalamu.

Hapa utapata taarifa za msingi na maelekezo ya tovuti za kuaminika zinazotoa mwongozo kwa wanafunzi wanaoazimia kufanya uandishi wa kitaaluma, kuepuka wizi wa maandishi, kutumia mitindo tofauti kama APA na AMA na kadhalika.


Haja gani kunukuu

Kwa nini inabidi tunukuu vitabu, majarida, tovuti na kadharika, tunazotumia katika maandishi ya utafiti? Sio tu sababu ya wizi wa maandishi!

Waandishi wote (wewe ukiwepo!) lazima wanukuu....

  • Kuonyesha umakinifu na ukamilifu ulioweka katika kazi ya kutafuta na kuchunguza vyanzo vyako.
  • Kama heshima kwa wasomaji wako.
  • Kukiri waandishi waliochangia na kuwezesha kukamilisha vipengele tofauti vya kazi yako. Kutotoa nukuu za kutosha ni sawa na kuiba maandishi.
  • Ili kuonyesha uadilifu wako na ujuzi kama mshiriki kuwajibika katika mazungumzo ya kitaalamu.

Jinsi ya Kunukuu

Wakutubi mara nyingi wanaulizwa "Je, nitayanukuu vipi makala, kitabu, jarida au mtandao nikiandika karatasi ya utafiti wangu?" Hakuna njia moja tu sahihi ya kunukuu kumbukumbu . Miongozo ya Kuandika (kwa mfano APA na AMA) hutoa maelekezo na taratibu za kuandika karatasi za utafiti.

Unapaswa kutumia mwongozo wa uandishi ili kunukuu ipasavyo.  Miongozo tofauti hutumiwa na taaluma tofauti au maeneo tofauti ya somo:

  • Mwongozo wa American Psychological Association (APA) hutumika katika Sayansi ya Jamii.
  • MLA (Modern Language Association) Handbook for Writers of Research Papers for the Humanities.Mwongozo wa (Modern Language Association (MLA ) hutumika katika Humanities.
  • Turabian (Chicago) Mwongozo kwa waandishi wa Historia.
  • Council of Science Editors (CSE) Mwongozo wa kisayansi kwa Sayansi.

Miongozo hii yote inapatikana katika maktaba Healey.  Vilevile, miongozo hii inayaweza pia patikana bure katika mtandao. Angalia viungo katika upande wa kulia. Hata hivyo maduka ya vitabu huuza miongozo ya mfukoni inayopendeza wanafunzi mara nyingi. Mojawepo ya miongozo maarufu ni Pocket Style Manual ilioandikwa na Hacker Diana (NY: Press St Martin, 2011)

Hakikisha kutoka kwa mwalimu wako kama huna uhakika wa mwongozo unopasa kutumia katika karatasi yako ya utafiti.

Academic Writing

Uandishi wa Akademia

° Purdue University's Online Writing Lab (OWL), usaindizi wa uandishi wa lazima kama:

° Healey Library Plagiarism Awareness and Prevention

 

 

Healey Library | University of Massachusetts Boston | 100 Morrissey Blvd | Boston, MA | 02125-3393 | 617-287-5900