Sehemu hii inatoa mwongozo wa kutumia mitindo tofauti kama APA na AMA katika uaandishi wa kitaalamu.
Hapa utapata taarifa za msingi na maelekezo ya tovuti za kuaminika zinazotoa mwongozo kwa wanafunzi wanaoazimia kufanya uandishi wa kitaaluma, kuepuka wizi wa maandishi, kutumia mitindo tofauti kama APA na AMA na kadhalika.
Haja gani kunukuu
Kwa nini inabidi tunukuu vitabu, majarida, tovuti na kadharika, tunazotumia katika maandishi ya utafiti? Sio tu sababu ya wizi wa maandishi!
Waandishi wote (wewe ukiwepo!) lazima wanukuu....
Jinsi ya Kunukuu
Wakutubi mara nyingi wanaulizwa "Je, nitayanukuu vipi makala, kitabu, jarida au mtandao nikiandika karatasi ya utafiti wangu?" Hakuna njia moja tu sahihi ya kunukuu kumbukumbu . Miongozo ya Kuandika (kwa mfano APA na AMA) hutoa maelekezo na taratibu za kuandika karatasi za utafiti.
Unapaswa kutumia mwongozo wa uandishi ili kunukuu ipasavyo. Miongozo tofauti hutumiwa na taaluma tofauti au maeneo tofauti ya somo:
Miongozo hii yote inapatikana katika maktaba Healey. Vilevile, miongozo hii inayaweza pia patikana bure katika mtandao. Angalia viungo katika upande wa kulia. Hata hivyo maduka ya vitabu huuza miongozo ya mfukoni inayopendeza wanafunzi mara nyingi. Mojawepo ya miongozo maarufu ni Pocket Style Manual ilioandikwa na Hacker Diana (NY: Press St Martin, 2011)
Hakikisha kutoka kwa mwalimu wako kama huna uhakika wa mwongozo unopasa kutumia katika karatasi yako ya utafiti.
° Purdue University's Online Writing Lab (OWL), usaindizi wa uandishi wa lazima kama:
° Healey Library Plagiarism Awareness and Prevention